WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA VIWANJA VYA BUNGE KUUAGA MWILI WA MH.NDITIYE.

13 Februari, 2021 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma, Mhandisi Atashasta Nditiye (52) aliyefariki jana Februari 12, 2021 katika hospitali ya Benjamin Mkapa alikokuwa akipatiwa matibabu. Mbunge huyo ameagwa leo (Jumamosi, Februari 13, 2021) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Akizungumza